Thursday, 19 July 2018
RASMI ALLISON BECKER ATUA LIVERPOOL KWA DAU NONO NA KUWA MLINDA MLAGO GHALI ZAIDI DUNIANI
Klabu ya Liverpool rasmi wamekamilisha usajili wa mlinda mlango wa AS Roma Allison Becker kwa kiasi cha pauni Milioni 67 kwa mkataba wa miaka sita baada ya tetesi za muda mrefu.
Mlinda mlango huyo anakamilisaha usajili huo na kufanikiwa kuwa golikipa ghali zaidi duniani na kuvunja rekodi za makipa kadha wa kadha akiwemo Gianluigi Buffon akihamia Juventus akitokea Parma 2001 pamoja na Ederson Moraels wa Manchester City akitokea Benfica 2017
Hivyo liverpool wanakamilisha usajili wa mlinda mlango huyo na kuzipiku Chelsea na Real Madrid zilizoonyesha nia ya kumsajili mbrazili huyo kwa siku za hivi karibuni.
Baada ya kukamilika kwa usajili huyo ni kuwa Liverpool watatoa malipo ya awali kiasi cha pauni milion 56 huku klabu yake Intercional ya Brazil kabla ya kujiunga na Roma italamba kiasi cha pauni milion 2.2 na malipo mengine yatategemea mafanikio ya mchezaji huyo ndani ya klabu ikiwemo katika ligi ya EPL, Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na UEFA Europa League.
Ujio wa mlinda mlango huyo ndani ya klabu hiyo umefanya mstakabali wa Lloris Karius pamoja na Simon Mignolet kubaki njia panda mpaka sasa kufuatia kiwango kibovu walichokionyesha kwa msimu uliyopita ikiwemo katika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment