Pages

Monday, 24 August 2015

VITA IMESHAANZA BARANI ULAYA NANI BINGWA? MASHABIKI MATUMBO JOTO











Utamu wa ligi mbalimbali duniani umeanza kutimua vumbi zikiwemo zile Ligi kuu tano bora Ulimwenguni ambazo ni ENGLISH PREMIER LEAGUE maarufu-EPL (England), LA LIGA (Spain), BUNDESLIGA (Germany), SERIE A (Italy) na FRENCH LIGUE 1 (France), hivyo kuongeza shauku kwa mashabiki kuona nani atakuwa bingwa tena katika ligi hizo msimu mpya wa 2015/16.


Katika ligi kuu ya Uingereza imeanaza ikiwa ni michezo ya tatu huku tukishuhudia bingwa mtetezi Chelsea akianza ligi hiyo kwa kusuasua baada ya kushinda mchezo mmoja sare moja na kufungwa mchezo mmoja hivyo kuwa katika nafasi ya kumi mpaka sasa katika ligi hiyo huku wakiwa wanalingana alama na Arsenal ambao wako katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi hiyo.

Wakati Chelsea wakianza kwa kuchechemea katika ligi hiyo kwa wapinzani wao Manchester City wameanza vyema kwa kupata matokeo katika michezo yao yote mitatu bila kurusu bao hata moja mpaka sasa huku wakiwa na mabao nane ya kufunga.

Kwa upande wa Manchester United nao wameanza vyema ligi hiyo baada kushinda katika michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja hivyo kujikusanyia alama saba mpaka sasa ikiwa sawa na Liverpool pamoja na Leicester City.

Aidha katika Ligi kuu ya Spain maarufu LA LIGA vigogo wa ligi hiyo FC Barcelona na Real Madrid  walicheza michezo yao wiki endi hii katika michezo hiyo tulishuhudia Fc Barcelona wakiibuka kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Athletic Bilbao huku Real Madrid wakilazimishwa sare tasa dhidi ya Sporting Gijon

Pia ligi ya Ujerumani maarufu Bundesliga imeanza kwa michezo kadhaa kuchezwa ambapo tumeshuhudia bingwa mtetezi Bayern Munich akiiibuka na ushindi mwembamba wa bao 2-1 dhidi ya TSG Hoffenheim Wikiendi hii.

Paris Saint German (PSG) wameanza vyema kutetea ubingwa wao katika French Ligue 1 baada ya kushinda michezo yake yote mitatu hivyo kuendeleza ushindi kwa asilimia hamsini katika ligi hiyo.

Baada ya kuondokewa na wachezaji wao nyota msimu huu akiwemo Carlos Tevez, Andre Pirlo na Arturo Vidal vijana wa Massimiliano Allegri.Junentus wameanza vibaya kwa kukubali kulala kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Udinese katika dimba la nyumbani.

Tuone kitu gani kitajiri katika msimu huu katika ligi hizo tano kubwa ulimwengu kwani ndiyo kwanza mbio hizo zinaanza.

0 comments:

Post a Comment