Madrid ambao walisafiri mpaka Estadio de Mestalla walikuwa wa kwanza kundika bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Ronaldo ambaye anafunga bao la 26 la La Liga msimu huu
Ronaldo(Real Madrid) akihamaki baada ya kukosa bao katika mchezo dhidi ya Valencia ambapo madrid walilila kwa kichapo cha bao 2-1 katika uwanja huo wa Estadio de Mestalla
Lakini baada ya muda mchache tu kipindi cha pili kuanza Valencia waliweza kusawazisha kupitia kwa Antonio Barragan's kunako dakika ya 52, ikiwa ni bao l;ake la kwanza la La Liga la kushambulia tangu Machi 2007
Vijana hao wa Nuno Espirito Santo's waliandika bao la pili kunako dakika ya 65 ya mchezo kupitia kwa Nicolas Otamendi baada ya kupokea mpira safi wa kona uliyochongwa na Dani Parejo's na kujitwisha kichwa safi kilichomsinda Iker Casillas na kuwafanya Valencia kuibuka na alama hizo tatu na kuwafanya sasa kupanda mpaka nafasi ya nne na kuwaondoa Sevilla katika nafasi hiyo
0 comments:
Post a Comment