Klabu ya Arsenal imecheza mchezo wake Ligi ya M,bingwa jana usiku dhidi ya FC Basel na kuibuka na ushindi wa bao 2-0 katika dimba lao la Emirates lakini kuna tukio la klabu hiyo kuvaa jezi ya UGENINI wakiwa katika dimba lao la Nyumbani pale EMIRATES.
Kwa mashabiki wengi walishangaa tukio hilo lakini kuna baadhi walitambua kuhusu suala hilo ambalo linatokana na sheria pamoja na taratibu za UEFA kwa lengo la kutoa utata kwa marefa wakati wa maamuzi uwanjani.
FC BASEL katika mchezo huo walikuwa 'ni wageni kwahiyo walipaswa kuvaa jezi za ugenini kitendo ambacho walikitekeleza lakini tatizo lilikuwa katika rangi ya jezi kati ya timu hizi mbili yaani Arsenal pamoja na FC Basel ambapo ukitazama kwa umakini ni kwamba FC Basel jezi ya nyumbani ni rangi nyekundu,bluu na nyeusi wakati ya ugenini ni nyeupe, zote zikiingiliana na Arsenal.
Hivyo kutokana na FC Basel jezi ya ugenini kuwa nyeupe sheria ya UEFA hairuhusu kwasababu jezi ya Arsenal ya nyumbani ni nyekundu lakini ina rangi nyeupe mikononi kitendo ambacho hakiruhusiwi kwa sheria ya shirikisho hilo.
Bila shaka tatizo hilo lilipaswa kuondolewa na FC Basel ambao walitakiwa kuvaa jezi chaguo la tatu lakini hawakuwa na chaguo hilo hivyo kupelekea Arsenal kuvaa jezi yao ya ugenini ili kuondoa utata huo.
Lakini kwa mashabiki wa Arsenal watakumbuka hii si mara ya kwanza kwa matukio kama haya kutokea kwa washika bunduki hao kwani lilitokea 1998 dhidi ya Lens ambapo walilazimika kuvaa jezi chaguo la tatu ili kuondoa utata kama huo.
Wakati huo ulikuwa katika ligi ya Mabingwa, mchezo uliyopigwa katika dimba la Wembley ambapo walivaa jezi chaguo la tatu rangi ya bluu huku Lens wakivaa jezi yao ya nyumbani ya rangi nyekundu na kijani baada ya ugenini kufanana na Arsenal.
Aidha tukio kama hilo lilitokea tena 1991 wakati huo mashindano haya yakifahamika kama Kombe la Ulaya(European Cup) dhidi ya Benfica,walipolazimika kuvaa jezi za rangi ya njano katika dimba la nyumbani.
Jambo pekee Katika matukio hayo yote Arsenal walipobadilisha jezi wakiwa katika dimba la nyumbani walipoteza mchezo huo,lakini suala hilo halikuweza kutokea usiku wa jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment