Pages

Sunday, 31 May 2015

BARCA WATWAA UBINGWA KWA COPA DEL REY KWA STAILI,IKIWA NI MIAKA 61 IMEPITA TANGU TIMU YA MWISHO IFANYE HIVYO










Barcelona wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey kwa staili baada ya kushinda michezo yote bila kupoteza mpaka kuwa mabingwa wa kombe hilo.


Tukio kama hilo halijawahi kutokea takribani miaka 61, tangu Valencia walipofanya maajabu kama hayo na kutwaa ubingwa  kwa kushinda kila mchezo wa kombe hilo ikiwa ni Mwaka 1954 ambapo Barcelona wamerudia msimu huu kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao.

Katika michezo tisa waliyocheza Barca wamefunga mabao 34 na kufungwa mabao 6 tu, huku nyota wao Lionel Messi ambaye kwenye fainali hiyo alitupia nyavuni mabao  mawili anafikisha mabao saba akilingana na Iago Aspas wote wakiwa na idadi hiyo.


Wakongwe wa Barcelona Iniesta(koshoto) pamoja na Xavi(kulia) wakiwa wamenyanyua kombe la mfalme baada ya kulitwaa kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao hivi karibun.










Barca mbali na kushinda michezo yote ya Copa Del Rey msimu huu siyo mara ya kwanza kwa timu hiyo kufanya tukio kama hili kwani miaka 89 iliyopita, ikiwa ni mwaka 1926 ulikuwa ni mwaka wa mwisho kwa Barca kufanya tukio kama hilo katika fainali waliokutana na timu hiyo hiyo ya Athletic Bilbao, hivyo historia imejirudia kwa mara nyingine tena.

Baada ya ubingwa huo, sasa Barca wanafukuzia kombe la tatu msimu huu ambalo ni Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, huku wakitakiwa kushinda mchezo wao wa fainali dhidi ya Juventus hapo Juni, 6 mwaka huu uko Berlin, Ujerumani.

Ikiwa Barca watafanikiwa kutwaa kombe hilo itakuwa ni mara ya pili kutwaa vikombe hivyo  vitatu kwa msimu mmoja katika historia ya klabu hiyo tangu walipofanya kama hivyo  miaka sita iliyopita, ikiwa ni mwaka 2009 chini ya Pep Guardiola ambapo waliweza kutwaa Uefa Champion League, La Liga na Copa Del Ray.


0 comments:

Post a Comment