Monday, 15 June 2015
JEZI MPYA ZA CHELSEA ZA MSIMU WA 2015/16 ZAVUJA MITANDAO YA KIJAMII
Jezi mpya za msimu ujao za Chelsea zimevuja katika mitandao mbalimbali ya kijamii kabla ya kutambulishwa ikiwa na wafadhili wapya ambao ni Yokohama wakichukua nafasi ya Sumsung baada ya kumaliza ufadhili wao.
Jezi ya chelsea nyeusi ugenini pamoja na nembo ya wafadhili wapya Yokohama
Jezi hizo mpya ambazo zimebuniwa na Adidas zimeonekana katika mitandao hiyo namna nembo ya wafadhili wapya itakuwa pamoja na utandu mwekundu na mweupe katika kola na mikononi.
Jezi za Chelsea za Ugenini za rangi nyeupe ikiwa na logo ya wafadhili wapya Yokohama
Chelsea waliingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Matairi ya Yokohama kutoka Japan ambapo watakuwa wakiingiza kiasi cha Pauni milioni 40 kwa mwaka,
Dili kati ya Chelsea na Kampuni ya Matairi ya Yokohama wa gharama ya Pauni 40 Mil kwa mwaka
Hivyo Kiasi cha fedha ambacho Chelsea wataingiza katika miaka hiyo mitano itawafanya kuwa timu ya pili kupata ufadhili nyuma ya Manchester United ambao wanavuna Pauni Milioni 53 kwa mwaka kutoka kwa Chevrolet.
Wachezaji wa Chelsea wakiwa katika moja ya ziara zao ikiwa kama sehemu ya kutafuta masoko zaidi
Aidha kutokana na dili hilo inawafanya Chelsea kuzimwaga klabu kubwa na tajiri duniani katika mikataba yao kama Real Madrid, Barcelona pamoja na Bayern Munichen.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment