Pages

Saturday, 2 May 2015

MAYWEATHER, PACQUAIO NANI MBABE? SWALI LINABAKI ULINGONI

Mchezo wa ngumi wa karne uliyokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa mchezo huo unatarajiwa kupigwa usiku huu katika ule ukumbi wa MGM Grand uliyoko Las Vegas, Marekani.


Mchezo huo unawakutanisha kati ya mabondia wawili ambao wanatamba katika ulingo wa ngumi duniani katilka uzito wa welterweight kati ya  Floyd Mayweather(38) na Manny Pacquiao(36),huku pakiwa bado pana sintofahamu nani ataibuka bingwa katika mchezo huo usiku huu.

Mayweather anakutana na mpinzani wake huyo huku akiwa na rekodi nzuri ya kucheza mapambano dhidi ya mpinzani wake huku akiwa amecheza mapambano 47 akishinda yote, huku Pacquiao akiwa amepigwa manne na kutoa sare mawili katika mapambano 64 aliyocheza mpaka sasa.

Wababe hao walikutana hapo siku ya Ijumaa katika .ukumbi  Vegas hullabaloo kabla ya pambano lao wakati wakipima uzito ambapo Mayweather uzito wake ni 146lbs, huku Pacquiao akiwa na uzito wa 145lbs, katika upimaji huo takribani mashabiki 16,000, walishuhudia tukio hilo.


0 comments:

Post a Comment