Pages

Monday, 8 September 2014

VITA YA NAMBA 9 REAL MADRID

Karim Benzema mwaka uliyopita ulikuwa rahisi sana kwake kikosini Real Madrid. Lakini ikiwa sasa mazoezi yanaanza upya huko Valdebebas, sasa yuko karibu kukutana na mtu mwenye jina kubwa: yaani Javier 'Chicharito' Hernández.


Wakati mchezaji huyo anaondoka siku kadhaa kwenda kuchezea Ufaransa, yeye  ndiye aliyekuwa mshambuliaji wa kati pekee katika klabu hiyo ya Real Madrid, ujio katika kikosi hicho wiki ijayo atakutana na upinzani mkali.

Real Madrid wataanza mazoezi jioni ili kuwapa muda wa kutosha wa kupumzika wale wachezaji waliyocheza michezo ya kimataifa ili kurudi kambini kwa wakati.

Benzema ni mmoja wao, wakiwemo pamoja na Varane, Kroos, James, Pepe na Coentrao. Hivyo itakuwa mara ya kwanza kati yake na Hernandez kukutana baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kusajiliwa dakika za lala salama katika dirisha la usajili lililofungwa. Watapeana mikono na kuanza vita ya namba 9 katika kikosi cha Real Madrid.

Benzema hakuwa katika upiganaji wa namba tangu alipoondoka Higuan kwenda kukipiga katika klabu ya Napoli ya Italia msimu uliyopita,ambapo klabu hiyo iliachana na maamuzi ya kumsajili mshambuliaji mwingine ambaye angempa changamoto Mfaransa huyo katika eneo hilo la mbele.

Kufika kwa Javier Hernández katika klabu hiyo akumaanishi kwamba Benzema atapoteza namba kwa muda huu mchache.Kwani kocha wa timu hiyo ya Carlo Ancelotti anamwamini sana na anamuhitaji mno kwasababu ni muhimu sana katika ule muundo wa BBC.Ambao unawajumuisha Cristiano Ronaldo na Gareth Bale zaidi ya mshambuliaji mwingine na hii ni kutokana na kufaa kwa Benzema na ambaye amekuwa akifanya vizuri sana katika muunganiko huo.


0 comments:

Post a Comment