Wednesday, 27 May 2015
SEVILLA WAKUWA MABINGWA WA KIHISTORIA UEFA EUROPA LEAGUE BAADA YA KUTWAA KWA MARA NYINGINE
Sevilla wamefanikiwa kutetea ubingwa wa UEFA Europa League kwa ya mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Dnipro huko Warsaw.
Dnipro walitangulia kupata bao dakik ya saba ya mchezo huo kupitia kwa Kalinic kabla ya Kryochiwak kuejesha kwa upande wa Sevilla huku Carlos Bacca akiongeza bao la pili kabla ya Dnipro kusawazisha na Bacca kuongeza bao la ushindi.
Hivyo Sevilla inakuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya kitendo kama hichi Mwaka 2006 na kutetea tena ubingwa huo msimu uliyofuata wa 2007 wakiwa katika kiwango bora kabisa.
Pia baada ya kutwaa ubingwa huu inaifanya Sevilla kuwa klabu ya Historia ya kombe hilo kwa kutwaa mara nne huku wakiwapiku Juventus, Inter Milan pamoja na Liverpool amabo wametwaa mara tatu kila mmoja mpaka sasa.
Matheus wa Dnipro's akitolewa nje kwa machela katika mchezo wa fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Sevilla baada ya kupata jeraha kichwani.
Katika mchezo huo tendo la mlinzi wa Dnipro,Matheu kutoka nje kwa machela kufuatia kupata mshtuko katika kichwa ikiwa ni dakika za mwisho za mchezo huo baada ya kugongana na mchezaji wa Sevilla ilizua hofu kubwa kwa wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hizo mbili katika dimba hilo lakini aliwezakupewa huduma ya kwanza na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi huku akiacha mchezo huo ukimalizika kwa Sevilla kuweza kutwaa ndoo hiyo kwa msimu huu ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Aidha kutokana na ubingwa huo inaifanya Sevilla kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao baada ya UEFA kuweka utaratibu huo ambao utaanza kutumika kwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo ya La Liga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment