Pages

Friday, 14 July 2017

BAKAYOKO AITEMA MANCHESTER UNITED AJIANDAA KUSAINI CHELSEA SAA 24 ZIJAZO
















Kiungo mkabaji wa klabu ya Monaco Tiemoue Bakayoko anatarajiwa kujiunga na klabu ya Chelsea ndani ya saa 24 kutoka sasa baada ya kuonekana akiwa na wachezaji wa klabu  hiyo akiwemo David Luiz na William katika moja ya mgahawa mjini London


Mchezaji huyo anatarajiwa kukamilisha usajili katika klabu hiyo kwa uhamisho unatarajiwa kuwa kiasi cha pauni milioni 40 ikiwemo nyongeza katika vipengele vya mkataba huo.

Aidha klabu ya Manchester United imekuwa ikitajwa kumfuatilia Bakayoko kwa ukaribu kabla ya mchezaji huyo kuamaua kujiunga, na mabingwa watetezi wa EPL, Chelsea ambao wanajiandaa na matembezi ya Singapore na China ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.


0 comments:

Post a Comment