Ikiwa hapo jana ni siku ya kuzaliwa kwa
mshambuliaji wa Argentina na FC Barcelona lionel Messi ambaye amefikisha umri
wa miaka 30, RAMADHANI KOKOTO.COM inakuletea rekodi pamoja na takwimu zake kwa
namba kama zifuatazo:
1: Bao la kwanza la
Messi katika kikosi cha wakubwa cha Barcelona ikiwa ni Mei Mosi 2005 akitokea
benchi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Albacete akiwa na umri wa miaka 17 tu
wakati huo.
2: Mfungaji wa pili
mwenye mabao mengi katika historia ya
mashindano ya ulaya ngazi ya klabu katika hatua ya makundi mpaka fainali.
3: Messi amefunga hat trick 37 akiwa na Barcelona.
4: Jumla ya medali
za ushindi za Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya maarufu UEFA
Champion league pamoja na makombe nane ya La Liga na Copa del Reys Tano
akiwa na Barca
5: Jumla ya mabao Lionel Messi
aliyefunga katika mchezo mmoja dhidi ya Bayer Leverkusen katika mashindano ya UEFA
Champions League hatua ya 16 mwaka 2012,
rekodi anayoshikilia pamoja na Luiz Adriano.
6: Messi amezifunga
klabu sita tofauti katika masindano ikiwa mwaka 2011 na kufanya hivyo tena 2015
7: Jumla ya Hat trick alizofunga za
mashindano ya UEFA Champions League akilingana na Cristiano Ronaldo).
8: Jumla ya
Mfululizo Wa misimu aliyofunga idadi ya mabao 40 au zaidi akiwa na Barca
9: Mabao pungufu kufikia idadi ya
mabao 100 kwa Messi katika kalenda ya mwaka 2012, akifikisha idadi ya mabao 91.
10: Messi alivaa
jezi namba 19 akianza kucheza katika kikosi cha Barcelona kabla ya kuja kurithi
jezi namba 10 mwaka 2008 baada ya
kuondoka kwa Ronaldinho's katika klabu hiyo
11: Messi alikuwa
karibu na umri wa 11 wakati bibi yake akiaga dunia kitendo kinachomfanya
kunyoosha vidole vyake angani anapofunga
12: Jumla ya mabao
ya aliyofunga akiwa na Argentina katika
kalenda ya mwaka, 2012, rekodi anayoshikilia pamoja na Gabriel Batistuta.
13:Umri aliondoka katika nchi yake ya Argentina na kuijunga na
FC Barcelona.
14: Namba ya mabao
aliyofunga Lionel Messi kwenye dimba la Santiago Bernabéu,huku akiwa wa pili dimba la Camp Nou katika ngazi ya klabu.
15: Jumla ya mabao
ya ugenini katika La Liga ndani ya msimu
mmoja, Pia anashikilia rekodi ya nyumbani kwa mabao 16
16: Messi alikuwa na
umri wa miaka 16 ,Miezi minne, na siku 23 wakati akicheza mchezo wake wa kwanza
katika klabu ya FC Barcelona dhidi ya FC Porto chini ya Jose Mourinho na
kutengeneza nafasi mbili za mabao
17: Rekodi ya mabao
aliyofunga katika ile Spanish Super Cup,
Misimu sita tofauti
18: Umri wa Messi
alipofunga bao lake la kwanza katika mashindano ya UEFA Champions League ,dhidi ya Panathinaikos.
19: Messi ni
mchezaji pekee kufunga timu 19 mfululizo katika La Liga
20: Messi amefunga
mabao 20 na zaidi dhidi ya timu sita
katika maisha yake ya mpira mpaka sasa ikiwemo timu sita za juu katika msimamo
wa La Liga msimu uliyopita
21:Mbio za ufungaji za muda mrefu za la liga
alizoweka katika msimu wa 2012/13, na kufanikiwa kufunga mabao 33 katika mfufulizo wa mechi hizo.
22: Umri aliyoweza kutwaa tuzo ya Ballon d'Or na FIFA World Player of the Year kwa kura nyingi
23: Jumla ya mabao aliyofunga
katika EL Clásico, ikiwa mabao matano zaidi ya Alfredo di Stéfano na saba zaidi
ya Ronaldo.
24: Umri ambao
alikuwa mfungaji wa muda wote katika klabu ya Barcelona.
25: Jumla ya fainali
alizocheza katika maisha yake ya mpira mpaka sasa.
26: ... Jumla ya mabao katika
fainali hizo
27: jumla ya mabao
aliyofunga kwa mipira ya adhabu maarufu free-kick kwa Barcelona.
28: Messi alikuwa
mchezaji mdogo kutoka bara la Amerika Kusini kufika michezo 100 ikiwa siku nne
kabla ya kufika umri wa miaka 28
29: Jumla ya mabao Messi
amefunga mpaka sasa dhidi ya Sevilla huku kwa Ulaya akiwa amefunga bao tisa dhidi ya Arsenal.
30 Umri wa sasa wa Lionel Andre Messi


0 comments:
Post a Comment